RASTAFARI UNITED
FRONT (RUF)
RASTAFARI BUSINESS FORUM (RBF)
Baraza la Biashara la
Rastafari
Rastafari United Front (RUF) kiutendaji ipo kwa asilimia 80
kiuchumi zaidi, asilimia 10 Kiutetezi na
asilimia 10 kijamii hivyo itawajibika zaidi kuwa na sera madhubuti za kiuchumi
mojawapo ni ile ya Baraza.la Biashara la Rastafari (RBF).
Baraza la Biashara la Rastafari (RBF) ambalo limesajiliwa
kama Bantu United Front (BUF) na BRELA na kupewa nambari ni utekelezaji
wa RUF wa mpango wa Umoja wa Afrika kufikia mwaka 2063 kuinua kipato cha ndani
cha mwananchi wa kawaida.
Lengo la RBF ni kuinua Jumuiya ya Rastafari kiuchumi na
kubadili mtizamo wake na waweze kuendesha na kumiliki uchumi wake yenyewe ulioimarika
na endelevu. RBF itawafanya Rastafari wawe na mwamko na kufuata kanuni bora za
kifedha na kuwa na shule, vyuo, hospitali, na ardhi yetu wenyewe kwa ajili ya makazi na kilimo na kuleta
ushiriki mkubwa zaidi wa Rastafari katika maendeleo ya Taifa kiuchumi.
RUF katika kazi yake ya kuunganisha Rastafari wote ina sera ya uchumi imara na endelevu
kuanzia ngazi ya wilaya, mikoa, kitaifa na kibara
Kazi hii ya kuunganisha imerahisishwa na Umoja wa Afrika (AU) kwani katika mkataba wake wa
Umoja na Utamaduni umechagua kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi ya
mawasiliano Barani Afrika.
Baraza la Biashara la Rastafari (RBF) litaweka mazingira ya
kuingia katika uchumi wa Bara bara la Afrika kwa kuzalisha bidhaa zinazotokana
na malighafi zetu na kuziwekea thamani na ubora utakaoshindana katika soko.
RBF inatoa fursa na mazingira ya ubunifu zaidi, kujiamini na
maarifa ya kiuchumi kwa kutoa elimu ya ujasiriamali ili azalishe bidhaa zenye
ubora na ushindani zaidi katika soko.
Sanaa kama muziki, sanaa za mikono, sarakasi, michezo,
vichekesho, uchoraji, uchongaji na n.k. ni kazi na inahitaji itumike kikamilifu
zaidi kama sehemu ya kuinua uchumi.
RBF itaweka mazingiza ya kutoa elimu ya ujasiriamali ili
kuzalisha bidhaa zenye ubora. Ili tuwe na uchumi imara na endelevu
ikishirikiana na mabaraza nchi jirani ya RBF ya katika kubadilishana uzoefu,
utaalamu na bidhaa zinazozalishwa katika nchi husika.
RBF itakuwa na ushirikiano na serikali ili kuweka mazingira
mazuri ya kulinda haki miliki za wasanii, usafirishaji bidhaa nje na ndani,
udhibiti wa bidhaa zisizo na viwango na ubora kuingia katika soko na unafuu wa
malipo ya ushuru n.k. RBF itahamasisha Jumuiya za Rastafari kuwa na ushirika wa
makampuni kama wanamuziki, wakulima, watayarishaji wa filamu na muziki, vyombo
vya habari na Televisheni, usafirishaji, utalii, ukandarasi, ufundi mekanika,
utunzaji wa mazingira, uvuvi na ufugaji n.k.
Hivyo mfumo wa utendaji kazi RBF utafanya kazi ya
kutengeneza mtandao kama utando wa buibui kwa
kwenda nchi zote Barani Afrika na kuweka msingi mmoja wa RBF Afrika.
No comments:
Post a Comment